Idara hii kwa usahihi inaitwa idara ya watoto na wanafunzi japokuwa imezoeleka kuitwa idara ya watoto.
Idara hii imeitwa hivyo kwa sababu idara hii inalea watoto kuanzia waliopo chekechea mpaka watoto wenye umri wa miaka 16.
Lengo kuu la idara hii ni kuwafundisha na kuwakuza watoto katika Neno la Mungu ili wawe wanafunzi wa Kristo.
Idara hi imelenga kuwakuza watoto katika maadili ya kiMungu ili waweze kumjua Mungu vizuri na hata baadae
kuweza kusimama wenyewe na kuendelea katika wokovu huku wakilikuza kanisa.