CASFETA

Wanafunzi wa CASFETA kutoka chuo cha Ardhi wakiongoza ibada ya sifa kwenye kanisa la TAG Mwenge

CASFETA ni kifupi cha maneno ya kiingereza “Christ Ambassadors Students Fellowship Tanzania”.
 
Huu ni ushirika wa vijana mabalozi wa Yesu walioko mashuleni na vyuoni. Lengo kuu la umoja huu ni kuwafundisha vijana Neno la Mungu na kuwahamasisha kumtumikia Mungu katika mazingira yao ya shule, vyuo hata nje ya mazingira hayo.
 
[Kitaifa idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa idara, akisaidiwa na makamu mkurugenzi. Wengine ni katibu wa idara na mweka hazina. Nafasi hizi nne pia zipo katika ngazi ya jimbo, ngazi ya sehemu na ngazi ya kanisa la mahali pamoja.]
 
Swahili