KANDA
Kuhusu kanda
Ili kuimarisha ushirika na umoja wa Kristo ndani ya kanisa na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa maono, malengo na majukumu mengine ya kanisa kama yalivyoainishwa, Tanzania Assemblies of God itagawanywa kijiografia katika kanda mbalimbali.

Malengo ya Mgawanyo wa Kanda
Malengo ya uanzishwaji wa kanda hizi ni pamoja na:
- Kuboresha utoaji wa huduma kwa makanisa, wachungaji na idara.
- Kusimamia miradi ya kanisa ya Kanda, mfano Vyuo mama vya Biblia, sekondari na redio.
- Kuimarisha ushirika na umoja wa roho ndani ya kanisa kwa kuwa na makongamano na semina za pamoja pale inapobidi.
- Kulikuza kanisa kiidadi, kijiografia na kiroho.
- Kanda zitakuwa na uwezo wa kuunda kamati ndogo ndogo za kusimamia miradi ya kanda pale itakapoona inafaa.
Viongozi wa Kanda
Kila Kanda itakuwa na viongozi wafuatao ambao watateuliwa na Kamati Kuu ya Utendaji na kuthibitishwa na Halmashauri Kuu:
- Mwenyekiti wa Ushirika wa Kanda atakuwa pia ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Chuo mama cha Kanda husika.
- Katibu/Mtunza Hazina wa Ushirika wa Kanda pia atakuwa ni Mkuu wa Chuo mama cha Biblia cha kanda husika.
Muda wa kazi kwa viongozi wa Kanda utakuwa miaka minne na uwezekano wa kuteuliwa tena na tena. Pamoja na kusimamia malengo ya Kanda kama yalivyoainishwa kwenye Katiba, viongozi wa kanda watafanya kila aina ya jitihada kusimamia ushirika na umoja ndani ya kanisa na pia watafanya kazi nyingine yoyote watakayopangiwa na Kamati Kuu ya Utendaji au Halmashauri Kuu.
Kwa maelezo zaidi Nunua katiba yetu sasa, Ili kununua