TAMKO KUHUSU USHOGA
Kanisa la TAG limetoa Rasmi Tamko kuhusu Ushoga. Ili kupata nakala ya tamko hili.Bofya Hapa

Idara ya Wanawake imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 20 sehemu ya 7 ya katiba ya Tanzania Assemblies of God. Hivyo kutokana na msingi huo Idara ya WWK imeandaa taratibu na muongozo wa Idara ya WWK kwa msingi wa kuongoza na kusimamia shughuli zote za Idara hii.
Kuwa na wanawake wa kanisa la TAG mbao ni jeshi halisi la Bwana Yesu, walio jaa nguvu za roho mtakatifu, wenye kasi yakueneza na kutegemeza injili ambao maisha yao na ya jamii inayowazunguka huwa bora kwa mjibu wa kanuni za kibiblia. Pia idara ya WWK ipo kwaajili ya kuwaunganisha wanawake wote wa kanisa la TAG kitaifa na kanisa la mahali pamoja kwa kuwakuza kiroho, kuwapandikiza maono na mzigo wa kutumika na kutoa mafundisho yatakayowawezesha wanawake katika kanisa ili kutimiza agizo kuu kwa kutenda na kutoa mali zao
Wanawake wanaotangaza Injili ni jeshi kubwa
Idara ya WWK ni moja kati ya idara za kanisa la Tanzania Assemblies of God inayohusika na kupanga na kusimamia shughuli za kimkakati za wanawake katika ngazi zote za kanisa. soma zaidi
Mnamo mwaka 2008, Mchungaji Dr. Barnabas Mtokambali alichaguliwa kuwa askofu mkuu wa awamu ya tatu ya kanisa la Tanzania Assemblies of God. Ndipo Mrs. Faraja Hamuli akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WWK. Pamoja naye, ilikuwepo kamati ya utendaji ambayo wajumbe wake walikuwa ni Mrs. Eshimendi Swai (Makamu mkurugenzi Mkuu), Mrs. Josephine Manda (Katibu Mkuu), Mrs. Neema seng'enge (Mtunza hazina Mkuu) na Mrs. Gladmary Mtokambali (mshauri Mkuu).
Idara ya WWK ni maalum kwaajili ya wanawake wote wa Tanzania Assemblies of God.
Tushirikiane pamoja katika kutekeleza mpango mkakati sisi kama Wanawake kwani kwa umoja na pamoja tutatenda makuu.
MKURUGENZI MKUU
MAKAMU MKURUGENZI MKUU
KATIBU MKUU
MHAZINI MKUU
Wanawake watumishi wa Kristo.
Hii ndio kamati kuu tendaji kitaifa katika idara ya WWK.
Kanisa la TAG limetoa Rasmi Tamko kuhusu Ushoga. Ili kupata nakala ya tamko hili.Bofya Hapa
Familia ya makao makuu ya TAG inachukua wakati huu kutoa taarifa ya msiba wa aliyekua Mkurugenzi Kuu wa Idara ya Elimu Kitaifa Rev. Jonas Mkoba uliotokea Tarehe 01 mei 2023.
Idara ya watoto na wanafunzi kitaifa inachukua nafasi hii kuwatangazia waliimu na viongozi wa Idara ya watoto wote wa kanisa la TAG kua wiki la Idara litaanza hivi karibuni. Hivyo basi watoto na wanafunzi wote wanasisitizwa kuhudhuria katika ratiba zote sawa sawa na walivyopangiana katika kanisa la mahali pamoja.
Kutakua na Mkutano Mkuu wa Vijana yaani CA's ambao utafanyika CBC Dodoma hivyo Vijana wote mnahimizwa kuhudhuria bila kukosa.