Mfuko wa Mafao wa Tumaini (TPF) ulianzishwa 01/01/2019 na kanisa la TAG ili kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watumushi wake.

Maono

Kuwa Mfuko wa mafao wa mfano kwa mifuko mingine ya ziada nchini

Dhima

Kutoa huduma bora ya hifadhi ya jamii kwa watumishi kwa kuzingatia misingi ya imani ya kanisa

Maadili

Uwazi, Uaminifu, Uadilifu, Uwajibikaji, Ubunifu, Kufanya kazi kwa kushirikiana na Huduma kwa wakati

0
0

Kusudi la msingi la pensheni ya uzee ni kumhakikishia usalama wa kipato mtumishi aliyeishiwa nguvu kwa sababu ya uzee. Mtumishi anapokea kipato kila mwezi.

Pensheni ya urithi inalipwa kwa wategemezi wa mtumishi mwanachama wa TPF aliyepoteza uhai. Mafao ya urithi yamekusudiwa kufidia upotevu wa msaada wa kiuchumi uliokuwa ukitolewa na mtumishi aliyepoteza uhai.

Pensheni ya ulemavu inalipwa kwa mtumishi aliyepoteza uwezo wa kufanya kazi kwa sababu ya ulemavu wa kudumu uliosababishwa na ajali au ugonjwa

Mfuko wa Mafao wa Tumaini (TPF) upo kwa ajili ya kukuhudumia wewe Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblies of God

Rev. Dktr. Barnabas MtokambaliAskofu Mkuu