Maono

Maono ya DMS ni kuwa chombo cha kutafuta, kutunza na kuakisi Uwepo na Utukufu wa Mungu kupitia huduma ya Muziki na Ibada.

Dhima

Idara ya DMS ipo ili kutunza uhai wa Kanisa kwa kuinua shauku na moyo wa Ibada iliyojaa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu

Makusudi

Kufanyika “mkono” wa ofisi kuu, kamati za majimbo, kamati za Sehemu na uongozi wa Kanisa la mahali pamoja kuwafundisha washirika wa TAG kumwabudu Mungu katika uzuri (ubora) na utakatifu.

Kuhusu sisi

Idara ya Muziki na uimbaji kitaifa ilianzishwa rasmi mwezi septemba mwaka 2021. Kama kitengo cha muziki na uimbaji cha kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa wa Idara hii wakati wa uongozi wa Askofu Mkuu wa TAG Dr.Rev. Barnabas Mtokambali. Uanzishwaji huu ulitoka na lengo mkakati (B4) la Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho, linalotoa ufafanuzi kuwa Idara ya muziki na uimbaji ianzishwe na kuanza kufanya kazi ...