Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake


Ijue Idara ya Umisheni

Vuguvugu la umisheni lilianza mwaka 1989 wakati wa mkutano mkuu wa TAG uliofanyika Jerusalem Temple Mbeya. Hapo iliamuliwa na Halmashauri Kuu kwamba TAG ipeleke wamishenari wa ndani Zanzibar. Vuguvugu hilo liliendelea mpaka Agosti 1996 ambapo kanisa la nchi liliamua kuanzisha Idara kamili ya Umisheni wakati wa uongozi wa awamu ya pili ya TAG chini ya Askofu Mkuu Ranwell Mwenisongole. Uongozi huo alimteua Rev. Oral Sossy kuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Idara. Mwenyekiti wa wamishenari Greg Beggs alipendekezwa kuwa Katibu na Mtunza Hazina huo ndio ukawa mwanzo wa Idara hii.

umisheni logo

MAONO

Kuwa idara bora, makini na yenye uwezo wa kutimiza AGIZO KUU la Bwana wetu Yesu Kristo kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19-20; Marko 16:15-20 na Mdo 1:8.

DHIMA

Kuandaa, kuwawezesha na kuwatuma Wamishenari ndani na nje ya nchi kwa makabila na mataifa ambayo hayajapata kusikia Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo ipasavyo.

MAKUSUDI

Idara ya Umisheni ipo kwa kusudi la kutekeleza dira ya Maendeleo/Mpango mkakati wa kanisa la nchi. Kwa kuuambia ulimwengu kuhusu Yesu Kristo na kwa kuwakuza waamini kwa ibada, huduma, ushirika wa kikristo na utoaji chini ya uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu.