Kuhusu kanisa la mahali pamoja

Makanisa ya mahali pamoja ni yale ambayo ni vikundi au kundi la waamini ambao wanakubaliana na imani na mafundisho ya TAG, ambao wanakutana mara kwa mara kwa ajili ya kuabudu kwenye eneo maalum walilokubaliana na chini ya uongozi wa mmoja wa watumishi anayetambuliwa na Kamati ya Sehemu, Jimbo au Kamati Kuu ya Utendaji. Makanisa haya yatakuwa na viwango au masharti kwa ajili ya ushirika ambayo yatawekwa na Baraza Kuu la TAG nayo yatagawanyika katika madaraja mawili: Makanisa machanga na makanisa yaliyokomaa.