Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho, Tunamtaka Bwana na Nguvu zake.

Kwa Umoja na Pamoja tutatenda Makuu

Kuhusu Makao Makuu ya Kanisa

Makao Makuu ya kanisa la TAG yanaweza kuwa sehemu yoyote ile ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama itakavyoamuliwa na Halmashauri Kuu na kuthibitishwa na Baraza la Waangalizi kwa kiasi cha kura ya theluthi mbili (⅔) ya wajumbe wote wa Baraza la Waangalizi. Hivyo basi mnamo tarehe 01/11/2021 Makao Makuu ya kanisa (ofisi kuu, Idara makao makuu pamoja na vitengo vyote) yalihama kutoka Ubungo-Dar Es Salaam na kuhamia Dodoma, hivyo basi huduma zote zinatolewa mkoani Dodoma yalipo makao makuu.