GLOBAL EVANGELISTIS TRAINING INSTITUTE – MAYANI, LINDI

Kuandaa, kuwezesha, na kukuza wainjilisti watumishi wenye elimu bora ya kipentekoste, ustadi, uadilifu na shauku ya kulizidisha kanisa na kuufikia ulimwengu na Injili kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

KUHUSU CHUO

Chuo au Taasisi hii ya Mfunzo ya Wainjilisti inatambulika kwa jina la Global Evangelists Training Institute. Chuo kipo Nchini Tanzania – Afrika Mashariki, katika Manispaa ya Lindi mkoani lindi. Chuo hiki kipo kwa ajili ya kuwa noa Wainjilisti ili kuongeza Ufanisi katika huduma na hivyo kupata Matokeo makubwa katika kazi na huduma ya Uinjilisti kwa ujumla.

Tangazo!!!

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Wainjilisti (GETI), Rev. Joel Mwasongwe anakukaribisha muinjilisti kujiunga na chuo kwa Mafunzo ya Wainjilisti. Muhula wa masomo utaanza Tarehe 04/09/2023.

  1. Mwinjilisti wa kitaifa Bofya hapa ili kupakua fomu.
  2. Mwinjilisti wa Kanisa,sehemu au Jimbo Bofya hapa ili kupakua fomu.
  3. Fomu ya mapendekezo Mwinjilisi wa Jimbo,sehemu au kanisa Bofya hapa ili kupakua fomu.

Jaza fomu kisha tuma kupitia taggeti2022@gmail.com au wasiliana nasi kupitia: 0742101010 / 0743641066 / 0685918115.

tangazo
MAADILI YA MSINGI
UTAKATIFU NA UADILIFU

Kila mtu katika Chuo atadhihirisha Uaminifu, Maisha Matakatifu , Uadilifu pamoja na nidhamu ya Kiroho katika maeneo yote.

UAMINIFU KWA BIBLIA

Kila mtu katika Chuo aamini kuwa, Maandiko ya Biblia yamevuviwa na ni mafunuo ya Mungu kwa mwanadamu na ni kiongozi kisichoshindwa wala kubadilika.

UWAJIBIKAJI

Kila mtu katika Chuo atakua wakili na mwaminifu kwa kufuata na kutii kanuni na sheria zinazomhusu. Atatakiwa kutumia fedha za Chuo kwa kuzingatia taratibu, maelekezo na makusudi yaliyowekwa. Hii ni pamoja na kutoa taarifa sahihi ya eneo husika.

SERA NA VIGEZO VYA UDAHILI

Kwa kuwa chuo hiki ni cha Kipentekoste, na kwa kuwa Malengo yake ni kuwaandaa Wainjilisti wanaotoka katika makanisa ya Kipentekoste, Wanaopaswa kusoma katika chuo hiki lazima wawe na sifa zifuatazo.

  • Awe ameokoka
  • Awe amethibitika kuwa ana wito wa Huduma ya Uinjilisti.
  • Awe amejazea na Roho Mtakatifu.
  • Awe ana Uwezo wa kutumia lugha ya Kiswahili au Kiingereza kwa kusoma na kuandika.
  • Awe tayari kufundhishwa.