Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake






Kuhusu Idara ya Uinjilisti

Huduma ya Uinjilisti ilianza rasmi Mwaka 1940 kupitia Wazee wetu (Wainjilisti watano); Rev Emmanuel Lazaro, Rev Moses Kulola, Rev Christian Kiwia, Ev Mathias Ng’andu na Rev Daudi Kuselya. Hawa walikuwa Wainjilisti wa mwanzoni kabisa ambao walihubiri kila kona ya Tanzania na kuhakikisha wanapanda makanisa ...Mwaka 2004, Idara ya Uinjilisti ilianzishwa rasmi katika kanisa la TAG, baada ya pendekezo la kuanzishwa kwake na kupitishwa na Halmashauri Kuu. Pamoja na mikutano Mikubwa ya Injili iliyofanyika huko nyuma, bado hapakuwa na chombo rasmi kitaifa cha kuratibu huduma hizi za Uinjilisti isipokuwa kulikuwa na Kamati tu zilizoundwa kwa kusudi husika la kuandaa mikutano hiyo mpaka mwaka 2004 ambapo Idara ya Uinjilisti Kitaifa ilipoanzishwa rasmi.

uinjilisti

DHIMA

Ni kuhakikisha Injili inahubiriwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, Kwa njia inayoendana na mazingira ili watu wa Tanzania na ulimwenguni kote wapate kusikia habari za Bwana na Mwokozi Yesu Kristo kwa lengo la kuwafanya wawe Wanafunzi wake.

KUSUDI

  • Kuhamasisha na kueneza huduma za Uinjilisti kitaifa.
  • Kuleta Uamsho na kutunza utakatifu ili moto wa Uamsho usizimike.
  • Kuibua na kuibua vipawa vya uinjilisti wa ngazi mbalimbali.

MAADILI

  • Uaminifu kwa Biblia.
  • Uadilifu.
  • Wajibu kwa jamii kwa kuonesha taswira ya upendo na haki kwa watu wote.
  • Kuvuna kwa pamoja.
  • Kuvuna Kimkakati.