Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Sisi ni nani?
Kanisa la Tanzania Asssemblies of God lilipoanza mwaka 1939 halikua na chuo chochote cha Biblia wala mafunzo yeyote rasmi yaliyotumika kuandaa Watumishi. wamishenali walihubiri Injili na watu waliokoka na miongoni mwa watu waliookoka waliosikia wito wa Uwalithibitishwa na viongozi na kuingia shambani na kumvunia Bwana mavuno. Baadaye ikaonekana kuna uhitaji wa mafunzo rasmi ya kuwaandaa Watumishi kwa ajili ya kulifikia taifa kwa Injili ya Bwana Yesu Kristo. Ndipo mnamo mwaka 1980 kamati kuu ya wakati huo chini ya Uongozi wa Mchungaji Emmanueli Lazaro (Askofu Mkuu), Mchungaji Enos Kameta (Makamu Askofu Mkuu) na Mchungaji Solomoni Mwagisa (katibu Mkuu) walikaa na kushauriana na WWamishenari waliokuwepo wakati huo na kwa pamoja walikubaliana kuwepo kwa Idara ya Elimu na huo ndio ukawa mwanzo wa Idara hii.

MAONO
Kua na viongozi watumishi waliojitoa kwa Mungu na neno lake, waliobadilishwa kiroho na kuongozwa na Roho mtakatifu, Ili kuyafikia na kuyagusa mataifa kimkakati na injili ya Yesu Kristo.
DHIMA
Kuandaa, kuwezesha na kukuza viongozi watumishi wenye elimu bora ya kipentekoste, ustadi, uadilifu na shauku ya kulizidisha kanisa na kuufikia ulimwengu na injili kwa nguvu za Roho mtakatifu.
MAADILI
|