Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zakeIjue Idara ya Casfeta

CASFETA ni jumuiya ya wanafunzi walio mabalozi wa Kristo Tanzania yenye malengo tangu kuanzishwa kwake. Ushirika huu ni hitaji la wanafunzi walioko shule za sekondari na vyuoni kumuabudu Mungu kulingana na imani ya Kipentekoste. CASFETA ilianzishwa mwaka 1992. Wazo lake lilianzia kwa viongozi wa Idara ya vijana wa TAG, yaani Christ’s Ambassadors (CAs). Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CAs, mchungaji Uswege Mwakisyala alikuwa ndiye Mwenyekiti wa kamati ya watu watatu. Askofu Mkuu wa wakati huo Mchungaji Ranwel Mwenisongole alijibu kwa barua yake ya tarehe 8/10/1992, kuikubali huduma hiyo ianzishwe na kusimamiwa na idara ya Vijana CAs. CASFETA ilipata Mkurugenzi mpya 2008, Mch. Dkt. Huruma Nkone ambaye katika uongozi wake iliendelea kukua na kuzifikia shule, vyuo na vyuo vikuu vingi hapa nchini Tanzania, ambapo hadi kufikia mwaka 2020 kumekuwa na matawi zaidi ya elfu mbili mia tisa (2,900) nchini kote. Bofya hapa kutembelea tovuti yetu

casfeta logo

Maono

Kuwa kizazi kinachotembea katika nguvu za Roho Mtakatifu na kuubadilisha ulimwengu kwa Neno la Mungu.

Dhima

Kuwafikia wanafunzi wote kwa Injili ya Kristo kimkakati na kuwajenga kiroho kwa njia ya Kuabudu, Ushirika, Kufuasa ili waweze kuwahudumia watu wote kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kusudi

Kuwafundisha wanafunzi kuyaishi maadili ya kikristo, kupiga vita matendo yote yanayoharibu jamii kama vile; Magonjwa ya zinaa, UKIMWI, Utoaji mimba, Ulevi, Utumiaji madawa ya kulevya, Ushoga, Usagaji, Ubakaji, pamoja na matendo mengine yote maovu.

VIONGOZI WA IDARA YA CASFETA KITAIFA

Habari za Hivi Karibuni

Matukio ya Hivi karibuni kwa mwezi huu

Mei

Tanzia

Familia ya makao makuu ya TAG inachukua wakati huu kutoa taarifa ya msiba wa aliyekua Mkurugenzi Kuu wa Idara ya Elimu Kitaifa Rev. Jonas Mkoba uliotokea Tarehe 01 mei 2023.

5 - 11 Jun

Wiki ya Idara ya Watoto na Wanafunzi kitaifa

Idara ya watoto na wanafunzi kitaifa inachukua nafasi hii kuwatangazia waliimu na viongozi wa Idara ya watoto wote wa kanisa la TAG kua wiki la Idara litaanza hivi karibuni. Hivyo basi watoto na wanafunzi wote wanasisitizwa kuhudhuria katika ratiba zote sawa sawa na walivyopangiana katika kanisa la mahali pamoja.

12 - 16 Jun

Mkutano Mkuu wa CA's

Kutakua na Mkutano Mkuu wa Vijana yaani CA's ambao utafanyika CBC Dodoma hivyo Vijana wote mnahimizwa kuhudhuria bila kukosa.