Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake


Ijue Idara ya Vijana

Jina la Idara ni Tanzania Assemblies of God - Christ's Ambassadors (CA's); Yaani ikiwa na maana ya Vijana mabalozi wa Kristo.'Kimsingi ni Idara ya Vijana'.

cas logo

MAONO

Maono ya Idara ya Vijana ni kua na Vijana:-

 • 1: Walio jaa Roho mtakatifu kikamilifu.
 • 2: Walio hamasika kihuduma.
 • 3: Wenye mzigo na uwezo wa kuvuna roho zilizopotea kwa ufanisi mkubwa.
 • 4: Kua na viongozi waaminifu na wawajibikaji katika ngazi zote.

DHIMA

idara ya Vijana wajumbe wa Kristo kwaajili ya: -

 1. Kuhamasisha vijana.
 2. Kuunganisha Vijana.
 3. Kulea vijana katika malezi bora.
 4. Kupandikiza vijana Mzigo na Maono ya; -
  • 1: Kuabudu kwa hiari yao baada ya kufundishwa umuhimu wa kumuabudu MUNGU.
  • 2: Kutumika kwa bidii na viwango vya juu.

MAKUSUDI

Makusudi ya Idara ni:-

 1. Kushuhudia.
  • Idara inawaandaa vijana kwa mafunzo mbalimbali na kuwahamasisha ili kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali waweze kufanya uinjilisti wenye Nguvu utawawezesha kuwaleta watu wenyedhambi kwa Yesu.