Tunaamini katika Utatu Mtakatifu yaani Mungu Baba Mungu Mwana Mungu Roho Mtakatifu







MAONO

Bofya ili kusoma

Maono yetu kama kanisa ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kitaifa na kimataifa wakibatizwa katika Roho Mtakatifu huku tukiwa na ibada za kiroho, mafundisho halisi na sahihi ya Neno la Mungu na hivyo kuongezeka makanisa.

DHIMA

Bofya ili kusoma

Tanzania Assemblies of God (TAG) ipo kwa ajili ya kumuabudu Mungu katika Roho na kweli, katika kuuambia ulimwengu juu ya habari za Yesu na kuwapeleka waamini katika kumjua zaidi Yesu kupitia sifa, kuabudu na neno chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.

MAADILI

Bofya ili kusoma

Uaminifu Kibiblia, Uadilifu, Kuwajibika kijamii, Ushirikiano kama timu, Uvunaji kimkakati, Uwezeshaji wa uongoziUkuhani kwa waumini wote, Uwajibikaji wa usimamizi wa fedha, Ukuaji kimkakati, na Ubora.

Historia yetu

Tanzania Assemblies of God (TAG) ilisajiliwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya Societies Ordinance ya mwaka 1954 na kupewa namba ya usajili SO. 6246.

Tanzania Assemblies of God ni kanisa lililotokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa Azusa, California nchini Marekani, mwanzoni mwa karne ya 20. Paul Deer ambaye awali alikuja kama mmishonari wa kujitegemea, na alianzisha Kanisa la Pentecoste Holiness Association (PHA) mnamo mwaka 1928 ambapo ibada ya kwanza hasa ya Kanisa hilo ilianza mapema mwaka 1929 huko Igale katika Wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya. Mnamo mwaka 1938 Derr alirejea Marekani na mwaka uliofuata 1939 alijiunga na Kanisa la Assemblies of God, na hivyo kuikabidhi kazi iliyokuwa imeanzishwa Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) mikononi mwa Genenral Council ya Assemblies of God Marekani. Na kuuomba uongozi huo wampeleke Mmissionari kwenye kazi hiyo kuilea wakati yeye akiwa likizoni.

Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya mwanzo kanisa lilisimamiwa na wamishonari wa kimarekani pamoja na wachungaji wa kiafrika wakati huo {Yohana Mpayo [Marehemu] na Petros) waliokuwa maaskofu chini ya Assemblies of God Mission. Kanisa liliendelea kuongozwa katika mfumo huo hadi mwaka 1967. Kanisa la kwanza kabisa la TAG lilikuwapo pale Igale wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya.Ni mwaka huo wa 1967, uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa kuongza Tanzania Assemblies of God (TAG) Kanisa hili liiingia hapa nchini kama matokeo ya uamsho mkubwa wa Kipentekoste uliotokea kule Azuza Marekani. Hivyo lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa ni kuwafikia wenye dhambi kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini. ili kutimiza lengo hilo ilikuwa lazima watendakazi shambani mwa Bwana waandaliwe tangu utoto.


Historia ya Uongozi

Historia ya Maaskofu Wakuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God

1967

Rev. Dkt. Emmanuel Lazaro

Alikuwa Askofu Mkuu kuanzia mwaka 1967 mpaka 1998

1992

Rev. Dkt. Ranwell Mwenisongole

Alikuwa Askofu Mkuu kuanzia mwaka 1992 mpaka 2008

2008

Rev. Dkt. Barnabas Mtokambali

Alianza kuwa Askofu mkuu mwaka 2008 hadi sasa