Vijana

CA's wa kanisa la TAG Kibaoni Dar es Salaam wakiingia kanisani tayari kwa kuadhimisha sikukuu yao hivi karibuni.

Idara hii inawahudumia vijana wa kanisa la Tanzania Assemblies of God. Idara hii ni maarufu kwa jina la “CAs” ambacho ni kifupi cha maneno ya kiingereza“Christ’s Ambassadors” yaani “Mabalozi wa Kristo”. Lengo kuu ni kuwafundisha vijana na kuwalea ili kuwa wanafunzi wa Kristo na kuwahamasisha kumtumikia Mungu.
 
[Kitaifa idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa idara, akisaidiwa na makamu mkurugenzi. Wengine ni katibu wa idara na mweka hazina. Nafasi hizi nne pia zipo katika ngazi ya jimbo, ngazi ya sehemu na ngazi ya kanisa la mahali pamoja.]
 
Swahili