Ushirika Wa Wanaume

Wanaume wa kanisa la TAG Mwenge wakiimba katika moja ya sikukuu yao ya kitaifa.

Huu ni ushirika wa wanaume wa kanisa la Tanzania Assemblies of God , uliopewa jina la kiingereza kuwa “Christian Men’s Fellowship”na kwa kifupi (CMF) yaani “Ushirika wa Wanaume”.

 

Kusudi kubwa la ushirika huu ni kuwaunganisha wanaume wote katika kanisa ilikumtumikia Mungu nakuitegemeza kazi yake katika huduma mbalimbali ndani ya kanisa na kwa jamii inayotuzunguka.

 

Ndani ya kanisa ushirika huu ni maarufu kwa jina la “Taifa kubwa”. [Kitaifa idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa idara, akisaidiwa na makamu mkurugenzi.

 

Wengine ni katibu wa idara na mweka hazina. Nafasi hizi nne pia zipo katika ngazi ya jimbo, ngazi ya sehemu na ngazi ya kanisa la mahali pamoja.

Swahili