Uongozi Wetu

Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God Rev. Dr. Barnabas Mtokambali (katikati), Makamu wa Askofu Mkuu Dr. Rev. Magnus Muhiche (Kushoto) na Katibu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God Rev. Ron Swai (Kulia).

 

UONGOZI

 

Mfumo wa uongozi wa Tanzania Assemblies of God uko kama ifuatavyo:

 

BARAZA LA WADHAMINI

Baraza la Wadhamini linajumuisha: Askofu Mkuu, Makamu Askofu Mkuu, Katibu Mkuu, na wajumbe wawili  waliochaguliwa na Halmashauri Kuu. Baraza hili litaitwa “Wadhamini Walioandikishwa wa Tanzania Assemblies of God”.

 

 

KAMATI YA UTENDAJI YA BARAZA KUU

Kamati ya utendaji itajumuisha: Askofu Mkuu, Makamu wa Askofu Mkuu, na Katibu Mkuu/Mtunza Hazina.  Muda wao wa kazi utakuwa miaka mine na uwezekano wa kuchaguliwa tena na tena.

 

HALMASHAURI KUU

Halmashauri Kuu itajumuisha: Viongozi walio kwenye Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu, Maaskofu wa Majimbo, Mwenyekiti wa Wamisionari wa Assemblies of God, na wajumbe wawili waliochaguliwa na Kamati ya Utendaji. Kipindi chao cha uongozi kitakuwa miaka mine.

 

 

BARAZA LA WAANGALIZI

Baraza la Waangalizi litajumuisha: Viongozi walio kwenye Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu, Kamati za Majimbo, Wakurugenzi wa Idara ngazi ya Taifa, Wamishenari wote wnaofanya kazi na Tanzania Assemblies of God, na Wakuu wa Vyuo vyote vya Biblia vya Tanzania Assemblies of God.

 

MABARAZA YA MAJIMBO

Mabaraza ya Majimbo yatajumuisha: Wachungaji wote katika majimbo husika  wenye vyeti vinavyotambuliwa na Tanzania Assemblies of God, Wakuu wa Idara katika Majimbo, na Wamishenari wa Tanzania Assemblies of God waliopo katika Jimbo husika.

Mpaka kufikia Juni 2015, Tanzania Assemblies of God ina majimbo 33.

 

 

MABARAZA YA SEHEMU

Ili kuweza kuwa na uongozi na utawala unaofaa, jimbo litagawanywa katika sehemu. Kila sehemu itamchagua Mwangalizi, Makamu Mwangalizi, na katibu/Mtunza Hazina.

Wajumbe wa Mabaraza ya Sehemu ni Watumishi wote wenye vyeti vinavyotambuliwa na Tanzania Assemblies of God, na Wakuu wa Idara za Sehemu husika.

Mpaka kufikia Juni 2015, Tanzania Assemblies of God ina sehemu 320

 

 

 

MAKANISA YA MAHALI PAMOJA

Makanisa ya mahali pamoja ni yale ambayo ni vikundi au kundi la waamini ambao wanakubaliana na Imani na mafundisho ya Tanzania Assemblies of God, ambao wnakutana mara kwa mara kwa ajili ya kuabudu chini ya  uongozi wa mmoja wa watumishi wnanotambuliwa na Baraza la Jimbo. Yatakuwa na viwango au masharti kwa ajili ya uanachama ambayo yatawekwa na Baraza Kuu la Tanzania Assemblies of God nayo yatagawanyika katika madaraja matatu: Makanisa machanga, Makanisa yanayoendelea. Na Makanisa yaliyokomaa.