Historia Yetu

 

 

HISTORIA FUPI YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD - MIAKA 75

 

Tanzania Assemblies of God ni Kanisa lililotokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa AZUSA, California (Marekani), mwanzoni mwa karne iliyopita ya ishirini. Deer ambaye awali alikuja kama Mmisionary wa kujitegemea, na alianzisha Kanisa la Pentecoste Holiness Association (PHA) mnamo mwaka 1928 ambapo ibada ya kwanza hasa ya Kanisa hilo lilianza mapema mwaka 1929 huko Igale, Mkoa wa Mbeya.

 

Mnamo mwaka 1938 Paul Derr alirejea Marekani na mwaka uliofuata 1939 alijiunga na Kanisa la Assemblies of God, na hivyo kuikabidhi kazi iliyokuwa imeanzishwa Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) mikononi mwa Genenral Council ya Assemblies of God Marekani. Na kuuomba uongozi huo wampeleke Mmissionari kwenye kazi hiyo kuilea wakati yeye akiwa likizoni.

 

Mwaka uliofuata 1940 Uongozi wa AG Marekani uliwasiliana na Mmisionari wake aliyekuwa nchini Kongo Ndugu Nilsen na kumwagiza aje Tanganyika ailee kazi ambayo Paul Derr alikuwa ameikabidhi AG.

 

Mmissionari Nilsen alifika na kuwakuta washirika hao wa Igale mwaka 1940, ambao walishirikiana naye kwa muda mfupi lakini walipogundua kwamba yeye ni wa AG na siyo PHA waliyokuwa wameizoea wengi wao walijitenga, mpaka alipokuja tena Derr nchini mwaka 1945 na kuwaleta tena pamoja baada ya majadiliano ya muda mrefu yaliyofikiwa mwaka 1948 na kisha akarejea tena marekani mwaka huohuo wa 1948.

 

Hata hivyo wale waliokubaliana na kuhamia kwa Paul Derr kwenye kanisa la AG waliwatafuta wa Missionarui wa AG waliokuwa Malawi (zamani hizo ikiitwa Nyasaland) kutaka ushirikiano wa kihuduma nao. Hii ilikuwa miaka mine baada ya Paul Derr kuacha na kurejea Marekani. Walitembea kwa miguu maili 120 kuwafikia wamissionari hao, hii ilikuwa mwaka 1952. Wamissinari hao walikubali na walifika Tanganyika mwaka huo huo. Na mnamo mwaka 1953 wakaanza kazi ya kuliimarisha kanisa na kulijenga kuwa la kienyeji (Indigenous church) kwa kuanzisha chuo cha Biblia cha Itende kwa lengo la kufunza watumishi kwa kazi za huduma. Kanisa la kienyeji ni Kanisa linalo jitawala, linalojieneza na linalojitegemeza lenyewe.

 

Zana na mikakati iliyootumika kuimarisha na kujenga kanisa ni: Vyuo vya Biblia, Machapisho ya ICI, Shule ya Jumapili (sasa Shule ya Uanafunzi na Maandiko), idara za CA’s na WWK.

 

Chuo cha Itende kilikoleza Uamsho kanda ya Kusini, na Chuo cha Biblia Arusha kilichoanzishwa mwaka 1959 kilieneza moto wa Uamusho mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodom,a, Mwanza, Tanga na Singida. Kwakweli vituo vikubwa vya uamusho vilikuwa viwili ambavyo ni: Mbeya kwa kanda ya kusini na Arusha – Masama kwa kanda ya Kaskazini, Kati, Ziwa, Tanga, na hatimaye nchi nzima.

 

Hapo 1952 wamissionari walipochukua uongozi wa kanisa walilisajili kama Assemblies of God Mission lakini 1967 walikabidhi uongozi wa kanisa kwa watumishi wenyeji. Kanisa tangu hapo likawa na Halmashauri kuu ya kwanza ya wenyeji inayojitegemea chini ya Askofu Mkuu aliyechaguliwa mwaka huo Mch. Emmanuel Lazaro. Hii ndiyo sababu Mchungaji Emmanuel Lazaro anajulikana kama Askofu wa kwanza mwenyeji wa TAG. Ijapokuwa kulikulikuwepo na maasjkofu wengine wenyeji yaani Mch. Petrosi na Mch. Yohana Mpayo hao ndio waliomtangulia Mch. Emmanuel lazaro, lakini hao walitumika chini ya Uongozi wa wamissionari wakati Kanisa bado ni Assemblies of God Mission.

 

Mchungaji Lazaro aliongoza kanisa la TAG tangu mwaka 1967 hadi 1992 (muda wa miaka 25). Mnamo mwaka huo (1992) Mchungaji Ranwell Mwenisongole alichaguliwa na Mkutano Mkuu kuwa askofu Mkuu na kuliongoza Kanisa la TAG tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2008 (miaka 16).

 

Mnamo mwaka 2008 mchungaji Mch. Dr. Barnabas Mtokambali alichaguliwa na mkutano mkuu wa wa Wachungaji kuliongoza Kanisa la TAG nafasi ambayo anaitumikia hadi sasa.

 

Miaka 75 ya uwepo wa Kanisa la TAG iliyosherehekewa mwaka jana (2014), inahesabiwa tangu wakati Mmissionari Paul Derr alipolikabidhi Kanisa kwa Baraza Kuu la Assemblies of God Marekani mwaka 1939 na ambao ndio wakati aposimikwa rasmi kuwa mtumishi wa AG na kanisa la Marekani na wala si wakati alipofika Tanganyika akiwa chini ya Kanisa la Pentecoste Holliness Asociation.