USHINDI SEMINARI YA CASFETA YAZINDULIWA

KATIKA kutekeleza Mpango Mkakati wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, ya Miaka Kumi ya Mavuno, kama ilivyoainishwa katika mwongozo wake, Jumuiya ya Wanafunzi waliookoka, wa Shule za Sekondari na Vyuo (CASFETA), imekuwa miongoni mwa idara zilizofanya vizuri kwa mpango husika unaoelekea ukingoni.
 
(Askofu mkuu wa TAG , Dk, Barnabas Mtokambali akipanda mti katika shule ya Ushindi Seminari ya idara ya Casfeta ya kanisa la TAG, Wengine ni baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio hilo.)
 
Jumuiya hiyo imekuwa miongoni mwa idara za kanisa hilo zilizoitikia wito kwa kuwa msitari wa mbele kufikia maono yaliyokusudiwa kwa kuamua kujenga Shule nzuri ya Sekondari huko, Kipalapala, nje kidogo ya Manispaa ya Tabora.
 
Hivi karibuni Askofu Mkuu wa Kanisa TAG, Dk.Barnabas Mtokambali, aliongoza umati wa watumishi wa Mungu, viongozi
wa serikali na wageni wengine waalikwa kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa shule hiyo iliyojengwa na Jumuia hiyo.
 
Askofu Mkuu wa TAG, Dr. Barnabas Mtokambali (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Tabora (Kushoto) Mkurugenzi mkuu wa idara ya CASFETA, Rev Huruma Nkone , wakielekea eneo maalumu la kukata utepe wakati wa tukio la uwekaji wa jiwa la msingi la shule ya Ushindi Seminari, wengine ni watu waliohudhuria tukio hilo.