KWA NINI WATOTO WAFIKIWE?

B.kuhudumia watoto huleta baraka za Mungu
 
Tunaona kwamba Mungu anatuagiza tuwafundishe watoto. Na Mungu huwabariki wenye kutii amri Zake. 
Mungu alimwambia Musa "Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha na kushika 
amri zangu zote sikuzote, WAPATE KUFANIKIWA WAO NA WATOTO WAO MILELE!" (Kumb 5:29). 
Katika mstari wa 33, Musa aliongeza maneno haya, "Enendeni njia yote aliyowaagiza BWANA , Mungu 
wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki." Ni 
lazima tutii amri za Bwana ili tuweze "Kufurahia maisha marefu" (Kumbu 6:2) kwa ujumla ni kwamba, 
tunaishi muda mrefu zaidi tunapotii Neno la Mungu
 
Mungu anataka kutubariki, Anatamani kubariki dunia yote. Ujumbe huo unarudiwa katika  Zaburi 67:1-2, hivi: 
" 1 Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.
 2 Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote."
 
Utii huleta baraka za Mungu , Tunapotii agizo la Mungu kuwahudumia watoto , Mungu atawabariki wao na 
sisi pia.