Idara ya wanawake

WWK wakiimba kwenye sikukuu yao hivi karibuni kwenye kanisa la TAG, Bethel Temple la Kijenge Arusha

Ushirika wa wanawake wa Tanzania Assemblies of God, ni maarufu kwa jina la WWK ambacho ni kifupi cha “Wanawake watumishi wa Kristo”. Kwa mujibu wa mwongozo wao, lengo kuu la ushurika huu ni kuwaunganisha na kuwahamasisha wanawake wa kanisa ta TAG ili waweze kumtumikia Mungu na kuitegemeza kazi yake katika huduma mbalimbali katika kanisa. Katika kanisa ushirika huu ni maarufu kwa jina la “Jeshi kubwa.”

Swahili